karibu sana


Welcome To Gidyne.blogspot.com ** Email: gidyne.blogspot.com .... To visit my Blog, go to ....www.gidyne.blogspot.com.....

I TRUST IN GOD

Saturday, 28 May 2016

Klabu ya soka yafungwa mabao 44 Ecuador

Klabu moja ya soka nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi mpya ya ufungaji mabao duniani.
Klabu hiyo ya Pelileo Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200.
Mshambuliaji wa Pelileo Ronny Medina alifunga mabao 18.
Rais wa Indi Native Diego Culequi amesema matokeo hayo hayakutarajiwa na wachezaji hawakuwa wamezoea joto kali ambalo anasema lilichangia kushindwa kwao.
Mwandishi wa habari Mwingereza Tim Vickery, ambaye amekuwa Brazil kwa miaka 20, amesema Bon Accord kwa sasa wamejadiliwa sana katika vyombo vya habari Ecuador.
Anasema ligi ya daraja la tatu ya Ecuador huwa na ushindani mkubwa.
Rekodi ya sasa inashikiliwa na Arbroath FC ya Scotland iliyofunga mabao 36-0 dhidi ya Bon Accord miaka 131 iliyopita.
Mwenyekiti wa Arbroath FC John Christison amesema ana wasiwasi kiasi kwamba rekodi yao waliyoiweka 1885 huenda ikavunjwa.
Amesema klabu hiyo itasubiri uamuzi wa Guinness World Records.
44-1
matokeo ya mechi kati ya Pelileo Sporting Club na Indi Native nchini Ecuador
18 mabao aliyofunga mshambuliaji wa Pelileo Ronny Medina
131 miaka ambayo rekodi ya sasa, Arbroath 36-0 Bon Accord, imedumu
Bw Christison ameambia BBC Scotland: "Ni rekodi ambayo tumeishikilia kwa miaka 130.
"Tutasikitika sana kama klabu iwapo tutaipoteza rekodi hii ambayo kama jiji twajivunia sana.
“Ilifahamika sana kwamba wakati huo kipa wetu hata hakugusa mpira na alisimama kwenye goli na mwavuli kwani mvua kubwa ilikuwa inanyesha.
"Lakini tutasubiri uamuzi wa maafisa wa Guinness.”
Siku hiyo ya ushindi wa Arbroath mwaka 1885, Dundee Harp walilaza Aberdeen Rovers 35-0.
Ingawa mwamuzi alisema mabao yalikuwa 37, karibu wa Dundee Harp alisema alirekodi 35 pekee, mabao ambayo mwishowe yalitambuliwa.
Mwaka 2002, mechi ya ligi kuu ya Madagascar ilitoa matokeo ya kushangaza baada ya mabingwa wateule AS Adema kulaza mahasimu wao wa jadi Stade Olympique I'Emyrne 149-0. Wachezaji wa Olympique walijifunga makusudi kwa hasira kulalamikia uamuzi wa refa.
@ BCC Swahili

Mourinho athibitishwa meneja mpya Manchester United


Jose Mourinho ametangaza rasmi kuwa meneja mpya wa klabu ya Manchester United.
Ametia saini mkataba wa miaka mitatu.
Mreno huyo anachukua nafasi ya Mholanzi Louis van Van Gaal, aliyefutwa kazi Jumatatu siku mbili baada ya kushinda Kombe la FA.
"José kusema kweli ndiye meneja bora zaidi wa soka kwa sasa," naibu mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward amesema.
Mourinho, 53, amesema: "Kuwa meneja wa Manchester United ni heshima kubwa sana katika mchezo huu. Ni klabu inayofahamika sana na kuenziwa kote duniani.”
Amesema amekuwa akihisi mvuto wa kutaka kuwa Old Trafford na kwamba daima amekuwa akisikizana na mashabiki wa United.
“Nasubiri kwa hamu kuwa meneja wao na kujivunia uungwaji mkono wao miaka ijayo.
“Kuna hisia fulani na upendo ambao huwezi kupata kutoka kwa klabu nyingine.”
Mourinho amekuwa bila kazi tangu afutwe na klabu ya Chelsea Desemba mwaka jana.
Mourinho ametia saini mkataba baada ya mazungumzo ya siku tatu baina yake, wakala wake Jorge Mendes na maafisa wakuu wa United.
Moja ya mambo ambayo anatarajiwa kuyafanya ni kumchukua mshambuliaji kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic, ambaye walifanya kazi pamoja wakiwa Inter Milan
@bcc swahili