MY FAMILY

MY FAMILY
MY BELOVED ONE

karibu sana


Welcome To Gideon Kifwete blog ** Email: gideyoh@gmail.com .... To visit my Blog, go to ....www.gidyne.blogspot.com.....

I TRUST IN GOD

Thursday 13 September 2018

MAISHA MAZURI NI YAPI? (What is the Good life?)



MAISHA MAZURI NI YAPI?
(What is the Good life?)
“Living well”
Je ina maana gan tunaposema kuishi vizuri,(maisha mazuri). Ina maanisha nini kusema maisha ni mazuri?
Kila mtu anapenda kuishi maisha mazuri hakuna anayependa kuishi maisha mabaya.Lakini swali hili si rahisi kama jinsi lilivyo.kuna namna nyingi jinsi wanavyo tafsiri kuhusiana na maisha mazuri.wengi wametafsiri maisha mazuri kama ifuatavyo
MAISHA YENYE MAADILI
Njia mojawapo tunayotumia kwa neno uzuri au nzuri.Ni kuthibitisha maadili mema au mazuri.Kwa hiyo tunaposema mtu anaishi vizuri au watu Fulani wanaishi vizuri tunakuwa tumemaanisha :-
Mtu mwenye kutia moyo,mstaarabu,mkweli,mwaminifu,mpole,anaesaidia wengine.wana fanya vitu vyote vyenye asili ya wema na ubinadamu.
Na hawatumii muda wao wote kufanya wanayoyapenda tu bali husaidia na wengine.Baadhi ya wanafalsafa wanasema ni bora kuishi maisha ya tabu wakati ukitenda mema kuliko kutenda mabaya.Kwamba mtu mwema ni yule anayepata tabu kiasi cha kufa kwa kutenda mema kuliko mtu tajiri ambae anatenda yasiyo faa.
Dini nyingi hutafsiri maisha mazuri ni yale yenye maadili mema na kuishi kulingana na amri za Mungu.Mtu anaeyeishi maisha haya hutii amri za Mungu na kufanya yanayostahili.Na huamini kuwa malipo ya wafanya mema yako mbinguni na yawafanya mabaya yapo hapa  hapa duniani au maisha baada ya kifo
MAISHA YA FURAHA
Kitu kinachofanya maisha kuwa na thamani ni kuishi maisha ya furaha.maisha ni kufurahi na kuburudika,mtazamo kuwa maisha ni furaha hufanya maisha kuwa na uthamani wake.
Mtu anaposema ana furaha ana maanisha anajisikia vizuri,na maisha mazuri yamefungamana na mfululuzizo wa kujisikia vizuri mda mwingi.maisha mazuri yanatakiwa kuwa ni yale yenye furaha.kuwa na marafiki wazuri na washauri wazuri husaidia mtu kuwa na furaha.
MAISHA YALIYO KAMILIKA
Kila mtu anahitaji kuwa na furaha ,tunathamini vingine kwa sababu vina maana kwa vitu vingine kwa mf:-
Tunathamini fedha kwa sababu hutusaidia kununua vitu tunavyo vihitaji.Baadhi ya watu huamini ukamilifu wa kila kitu katika maisha huleta kuwa na maisha mazuri,mf gari,nyumba, watoto n.k,kuna tatizo katika kufikiria katika mtizamo huu.Kuna watu wana ishi maisha ya burudani/starehe wakati wote, je tuwahesabu kuwa wanaishi “maisha mazuri”?.Wanafalsafa wengi wanakubaliana kwanza kwamba kuishi maisha mazuri kwanza ni lazima mtu awe na tabia njema ,au utu wema.Na pia hatuwezi kusema mtu anaishi maisha mazuri kama anapatwa na matatizo au shida mara kwa mara. Na sio tu vile mtu anavyojisikia yeye mwenyewe kuwa na furaha.Kuna baadhi ya mitazamo  ina bidi iwepo ili kuhesabu mtu ana maisha mazuri mf:-
AFYA: Binadamu lazima afurahie afya bora na kuishi muda mrefu.
MARAFIKI: Binadamu lazima awe na marafiki wazuri,kawaida ya binadamu ni kuhusiana na wengine kwa sababu hiyo kuwa na marafiki ni jambo la muhimu sana.
Ni lazima mtu kupata heshima kutoka kwa wengine bila kuangalia hali wala jinsia ,kuwa maarufu na mtu mwenye sifa sio kitu cha lazima.Uthamani wa mtu haupimwi kwa umaarufu alio nao,bali hupimwa na kutambulika na watu wanao mzunguka.
Ni muhimu kufanya yale yaliyomo kwenye uwezo wako,na kitu kitu kinacho mtofauticha binadamu na wanyama wengine ni juu ya kufikiria na kufanya maamuzi,kwa hiyo maisha mazuri pale mtu pia anapofanya yale yaliyopo ndani ya uwezo wake katika kuyafanya na kuyatenda.
MAISHA YENYE MAANA
Tafiti nyingi zimeonesha kuwa watu wenye watoto sio wote wenye furaha,ukilinganisha na wale ambao hawana watoto.Wakati wa ukuaji wa malezi kwa mtoto hasa pale watoto wanapofikia umri wa kupevuka wazazi huwa na kiwango kidogo cha furaha na huongeza kiwango cha mawazo.Japo kuwa na watoto ni kigezo cha kuwa nafurha lakini haifanyi kuwa chanzo cha maisha yenye maana.Wakati wa zamani kuwa na watoto wengi ilikuwa ni kitu cha kujivunia tena chenye ufahari lakini pale tu inapotokea kila mtoto kufanikiwa katika njia yake pale fahari hujitokeza lakini pia sio maana halisi ya kuwa na maisha mazuri.
Wagiriki wana msemo kuwa “usimuite mtu ana furaha mpaka awe amekufa” Huwezi kusema mtu ana furaha mpaka mtu huyo maisha yake yawe yamefika kikomo,haijalishi mtu ana furaha kiasi gani kwa sasa kitu kibaya chaweza kumtokea na kuharibu furaha yake.Mtu kumuhesabu kuwa na furaha ni mpka pale tutakapoona mwisho wa maisha yake umeishaje.”heri mwanzo mbaya kuliko mwisho mbaya”
Jimmy savile,Ni mtangazaji  wa BBC aliyekuwa na umaarufu mkubwa na watu walimpenda sana kutokana na kazi yake na aliipenda kazi yake alifanikiwa sana kutokana na kazi yake,alikuwa na marafiki wengi na watu walimheshimu.Lakini baada ya kufa ili fahamika kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa akiongoza genge la uzalilishaji wa kijinsia hasa kwa watoto.Kwa hiyo mbele ya watu alionekana kuwa ni mtu mwenye maisha mazuri lakini mwisho wa kifo chake ikafahamika alikuwa na makosa ya udhalilishaji wa kijinsia(serial sexual predator).Yamkini alifurahia maisha yake,Lakini ukweli hakutaka kusema kuwa alikuwa anaishi maisha mazuri au la.UKWELI MAISHA MAZURI NI YALE YAKUPENDEKA  NA YANAYOHITAJIKA KATIKA KILA NYANJA  AU YOTE YALIYOELEZWA HAPO

No comments:

Post a Comment