MY FAMILY

MY FAMILY
MY BELOVED ONE

karibu sana


Welcome To Gideon Kifwete blog ** Email: gideyoh@gmail.com .... To visit my Blog, go to ....www.gidyne.blogspot.com.....

I TRUST IN GOD

Friday, 17 November 2023

ROHO YA MWANADAMU KUWEZESHWA


ROHO YA MWANADAMU KUWEZESHWA!

*ILI ROHO YA MWANADAMU IWEZE KUTENDA KAZI KWA VIWANGO VYA JUU, NA KATIKA LIMWENGU ZA KIROHO;  SHARTI IWEZESHWE*

*_Human spirits are to be enhanced, for them to operate in higher dimensions, and in some spiritual realms_*

*ʍաӀ Թɾօօ*
+255762879363
+255718922662

*YALIYOMO/CONTENTS*

1⃣ *UTANGULIZI*
2⃣ *KANUNI YA UUMBAJI/CREATION AND ITS ORDER*
💿Roho za mbinguni
-Maserafi
-Makerubi
-Ofanini
-Malaika
💿 Malaika waasi & Mapepo (Majini)
💿 Roho za wanadamu
3⃣ *TAFSIRI YA ALAMA ZA LUGHA YA ROHO (ENCODING/DECODING OF THE SPIRITUAL LANGUAGE)*
💿 Kwa nini lugha ya kiroho ni ya mafumbo?
4⃣ *NAMNA GANI ROHO INAWEZA KUWEZESHWA/WHAT TO DO, SO AS TO RECEIVE THIS ABILITY?*

1⃣ *UTANGULIZI*

Haleluya kwa BWANA, Mpendwa unayefuatilia mafundisho ya rohoni ya Mwl Proo, ili kuongeza maarifa na ufahamu wa rohoni sasa tumefikia mahali pazuri pa kuchimbua vilindi (depths) vya kiroho. Zaburi 42:7 inasema 👉🏾 *Deep calls to deep*, waliotasfiri kiswahili hususani (SUV), wameandika "Kilindi chapigia kelele kilindi", haijanoga sana, lakini ili kuyapata ya kilindini sharti uwe kilindini; ukiwa kilindini, kilindi chenyewe kitayaita yanayopatikana huko vilindini. Hivyo nakukaribisha upate mlo wa kilindini, sio watu wote somo hili laweza kuwafaa (Ebrania 5:12-14). Kama mtu hajazoea kusoma documents zenye vitu vya kiroho sana, au hana uzoefu wa kiroho (personal spiritual experiences), anaweza  kutatizika. Nakushauri usome kama unapenda maarifa, kama unatamani kuwa na maisha ya kiroho binafsi yenye uzoefu wa kiroho mara nyingi, hakikisha unasoma. Kama unatamani kutumika kwa viwango vya juu vya kiroho katika safari yako ya utumishi, jenga msingi huu mapema, hakikisha unasoma sasa neno kwa neno. Na kama unaona bora uishi tu *ordinarily/kwa kawaida*, unaenjoy kuwa *church goer* pekee, huna vitu vya kiroho vya kuonesha unatembea na Mungu kwa viwango, basi fanya kuliacha. Nimeweka mawasiliano yangu ili jambo lisiloeleweka niulizwe. Tazama haya nimeyapeleleza ndivyo yalivyo, yasikie, uyajue, ili upate mema (Ayubu 5:27).
KARIBU

2⃣ *KANUNI YA UUMBAJI (CREATION & ITS ORDER*

🎴 *Leo natamani kwa sehemu tufahamu siri hizi za uumbaji. Najua desturi zetu za kujifunza zilitufunga namna yetu yakujifunza haikutupa kufahamu baadhi ya vitu. Mfano watu wengi wanaelewa mbinguni Mungu aliumba malaika tu, kumbe kwa viumbe vya mbinguni malaika ni moja tu viumbe wengi, na malaika nao waliumbwa wa aina nyingi.*

🎴 Uumbaji kilikuwa kitu cha rohoni zaidi kuliko huku nje, yaani Mungu ambaye ni Roho alikuwa amekwisha umba vingi rohoni kabla ya udhihirisho wake huku nje. Mfano wanaosoma vyanzo kadha wa kadha vya kiyahudi, wanaweza kujua hata wanyama ambao tunasoma literally katika Mwanzo 2:19-20, kuwa Adamu alietewa awape majina, tayari walikuwa na majina hayo katika roho, Adam kwa roho ya ufahamu aliweza kuyataja majina yao, 👉🏾 *_"and whatsoever Adam called every living creature, that was the name thereof"_* (Mstari wa 19b). Alikuwa akimwona 🦒, anamjua huyu ni twiga, akimtaja jina lake likawa ndilo hilohilo. Kabla ya Mtu kula tunda, aliona na kufahamu mambo kiroho zaidi ya kimwili (Mwanzo 3:6). Sasa Mungu ambaye ni roho aliumba roho kwa makundi mawili; roho za mbinguni na roho za duniani 👉🏾 {celestial spirits/spirits of heaven & terrestrial/earthly spirits}. Roho hizi zinatofautiana sana uwezo kulingana na matumizi na kusudi la kuumbwa kwake. Viumbe hivi vya roho viliumbwa vikiwa namna yake ya asili na utukufu *(proper domain/code of creation).*

🎴 Viumbe hivi haviwezi fanya kazi ambazo havikuumbiwa, au havikuwekewa uwezo husika muda wa kuumbwa kwake. Ni kama ambavyo Mbuni/Ostrich ni ndege, ila sio ndege wa angani, sio kwamba ni mzembe kuruka ila hiyo ndiyo *proper domain* ya kuumbwa kwake, hata kama kutatokea dharula akaruka kwa umbali fulani, atatua akiwa kachoka na maumivi tele, wakati ndege wengine wanaweza safiri wakahama nchi kabisa 👉🏾 🦅 🦅 🦅. Hivyo sasa roho au viumbe wa rohoni waliumbwa wakiwa na uwezo wa mambo kadhaa *(built-in abilities)*, mwanadamu naye ni roho kama viumbe vile vya rohoni, ila roho ya mwanadamu haikuwezeshwa kwa uwezo sawa na viumbe vya rohoni. Roho yake iliwekewa limitations/vizuizi kwa sababu ali-dizainiwa kama *terrestrial spirit* akae ndani ya mwili aishi duniani (Zaburi 115:16).

*I.) VIUMBE VYA ROHO ZA MBINGUNI*
_(spiritual creatures )_

Kama leo utapata neema ya kutwaliwa kwenda mbinguni kiroho (translated by the Spirit to heaven), haya utayakuta hivi. Katika kiti cha enzi cha Mungu 💺, kuna wanaomzunguka kwa order maalum (Zaburi 89:7). Mungu aliumba Maserafi (Seraphs/Seraphim), Makerubi (Cherubs/Cherubim), Ofanini (Ophanin), Malaika (Malaika wakuu/archangels, Malaika walinzi/Watchers of heaven, malaika wakuu wa miji ya dunia, Malaika walezi/walinzi wa watu (Guardian Angels), haya ni makundi makuu ya viumbe wa mbinguni (spirits of heaven) aliowafanya Mungu, hilo baraza la watakatifu hawakuumbwa mbinguni, ni wanadamu wachache waliowahi kutembea na Mungu kwa kiwango cha juu sana wakiwa duniani, wakainuliwa mpaka mbingu ya tatu wakapewa kusimama karibu kabisa na Mungu (Zechariah 3:7), wako ambao mimi Mwl Proo nafahamu wapo, ila sitawataja hapa kwa sababu watu wanaweza kuhoji chanzo cha taarifa, na ni cha ajabu hivyo tuendelee katika kuchambua kundi moja baada ya jingine.

🧚🏻‍♂ *MASERAFI/SERAPHIM*

🎴 Hii ndio inayosadikiwa na vyanzo vingi vya kiyahudi, kuwa ndiyo rank/cheo ya juu ya viumbe vya roho vya mbinguni. Niseme mambo kadhaa, mimi pia kwa roho ya ufahamu nimejua kwa kufunuliwa kuwa hawa ndio rank ya juu kabisa (Efeso 3:3). Nilipokuwa nikisoma Biblia nikakuta ni nabii mmoja tu Isaya (Isaya 6:2, 6), ndiye amewataja hawa Maserafi. Sifa alizozitaja zimewatofautisha na viumbe wengine, sifa moja kuu ni mabawa sita. Ezekiel aliona viumbe hawa wa mbinguni, lakini aliowaona walikuwa na mabawa manne (Ezekiel 10:21), na akaweka wazi kuwa ni Makerubi, Sifa za Makerubi katika Ezekiel wanafanana na wenye uhai wanne katika Ufunuo wa Yohana, lakini idadi ya mabawa ya wale viumbe katika Ufunuo 4:8 ni mabawa sita kama Maserafi. Mungu alinipa siri ya hawa maserafi kutotajwa sana katika maandiko, kwamba hakuwaumba kwa ajili ya dunia, wala kuhudumia wanadamu, nafasi yao haina uhitaji hata kutembelea dunia, hakuna mtu anaweza kuona Serafi asipokuwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, unaweza kuwaona kama umemwona Mungu, maana wao wapo juu ya kiti cha enzi 👉🏾 💺 (Isaya 6:2), Sio kwamba wamekikalia, La! Hasha! Hivyo hutasikia katika maandiko wala katika shuhuda zozote mtu kuona maserafi nje ya pale katika kiti cha enzi, hiyo ndiyo sababu kuu ya kutowaona katika simulizi zozote za dini ya kiyahudi. Kwa ujumla hawako involved kwa human affairs, kilichomfanya Serafi mmoja ahusike kutwaa koleo na kuchukua kaa la mawe toka katika madhabahu iliyo mbele ya kiti cha enzi, ni kwa kuwa huyu visitor Isaya Ben' AmoZ kafika pale akiwa hana viwango, lakini hawa hwahusiku na kuhudumia wanadamu (That's their proper domain).

🧚🏻‍♂ *MAKERUBI/CHERUBIM*

🎴 Hii ni aina ya pili ya viumbe vya roho vy mbinguni. Hawa wametajwa sana katika maandiko tangu kitabu cha Mwanzo mpaka vitabu manabii. Maandiko zaidi ya matano katik Biblia yameandikwa, "Wewe ndiwe Mungu uketiye juu ya makerubi". Ambapo katika kingereza pameandikwa *Between the cherubim*, hivyo unaweza pata mpangilio mzuri wa pale kwenye kiti cha enzi. Katika desturi za kiyahudi (Jewish traditions) hawa walijulikana sana, ni wazi kwamba kulikuwa na wengi katika mababa wa taifa la Israel waliwahi kuwa na experience ya kuwaona. Hata Musa alipopokea maelekezo namna ya ku-design Patakatifu pa patakatifu (Most Holy Place) ndani ya hema ya kukutania na kutengeneza makerubi (model cherubs) hakushangaa yeye wala waisrael, maana walijua hivyo viumbe vya mbinguni. Sasa viumbe hawa wanaweza kuhusika na mambo mengi tu ya wanadamu. Na Biblia inatuthibitishia hilo, kerubi aliwekwa ku-block path/entrance 🧚🏻‍♂🗡 ya njia ya kimwili (physical) inayoungana na ya ulimwengu roho kuiingia Eden bustani ya Mungu (Kuna siri nyingi hapo, hata kama Adamu au watoto wake wangetamani kurudi Eden waichungulie, wasingeiona hata bila hata yule kerubi kuwakata kwa panga).

🎴 Huyu ambaye anaitwa Mwovu, Ibilisi na Shetani hakuumbwa kwa lile daraja la juu la Maserafi, yeye alikuwa katika kundi hili la pili la Makerubi (Ezekiel 28:14). Aliumbwa akawa in charge wa majukumu kadha wa kadha ya mbinguni na duniani (Isaya 14:13-5). Ikumbukwe yale niliyoelezea katika somo lililopita kuwa sura hizi zinaongelea miji ya Tiro na Sidoni, na taifa la Babel, lakini nilieleza kwa namna gani imehusianishwa na Shetani, jitahidi upate somo lisemalo *NENO LA MUNGU NI UFUNUO*,

🎴 Pia tumeona maumbile yao hawa kama walivyoelezewa na Ezekiel (Ezekiel 10:10-21), sura zao, miili yao, mikono yao, idadi ya mabawa, idadi ya macho na kila kitu. Ila pia wanaweza kutokea wakiwa wamebadilika maumbile.

*NB*
*_VIUMBE HAWA WA ROHO ZA MBINGUNI (SPIRITS OF HEAVEN), WANAO UWEZO WA KUCHUKUA MAUMBILE MENGINE KATIKA UUMBAJI WA MUNGU, WAKAJIVIKA MIILI HIYO KWA MAKUSUDI FULANI (INCARNATION), HII NI ~BUILT-IN ABILITY~ KWA VIUMBE VYA ROHO WA ASILI YA KUWA ROHO ZA MBINGUNI, NDICHO HASA ALICHOKIFANYA SHETANI KATIKA MWANZO 3:1, INGAWA KWA ASILI YAKE HANA UMBO LA NYOKA (UFUNUO 12:7-12 IMEZINGATIWA), SHIKA HII TUTAITUMIA HUKO MBELE_*

🎴 Shetani katika ule mpango wake kuwaza kumpindua Mungu, hakushawishi Serafi hata mmoja, naam hakushawishi hata makerubi wenzake, kama alijaribu kushawishi hakumpata hata mmoja, alishawishi malaika ambalo ni daraja la chini zaidi (Ufunuo 12:4). Kama kungekuwa na Makerubi kadhaa ambao wangeungana naye basi kungekuwa Shetani wakuu kadhaa, maana wangelingana mengi na hao wengine. Najua unahoji kitu hapo, kwamba hawa sio malaika? twende polepole utayaelewa haya vyema.

🧚🏻‍♂ *OPHANIN (THE WHEELS)*

🎴 Hili ni kundi la tatu la viumbe wa roho za mbinguni, maana ya jina lao ni Magurudumu. Kwenye Biblia wametajwa kwa kificho kidogo, lakini katika maandiko ya kale ya kiyahudi (Ancient Jewish Writings) wametajwa sana. Sasa katika Ezekiel 10, hii Annunciation ya hapa ilihusisha kutembelewa na makundi haya mawili ya viumbe vya rohoni. Tusome maandiko haya hapa chini :-

*(Ezekieli 10 )*
------------
*13 Na magurudumu hayo yaliitwa Kisulisuli, nami nalisikia.*

*14 Kila mmoja alikuwa na nyuso nne; uso wa kwanza ulikuwa uso wa 🧚🏻‍♂  kerubi, na uso wa pili ulikuwa uso wa  🧑🏻 mwanadamu, na uso wa tatu ulikuwa uso wa 🦁 simba, na uso wa nne ulikuwa uso wa 🦅 tai.*
...
*16 Na makerubi walipokwenda, magurudumu yale yalikwenda kando yao; na makerubi walipoinua mabawa yao, wapate kupaa juu kutoka katika dunia, magurudumu yale hayakugeuka wala kutoka kando yao.*

Mstari wa 14, umeongeza kitu cha ajabu, katika Ufunuo sura ya 4, wenye uhai wanne wako exactly sawa na Makerubi, wa Ezekiel 10, lakini kule aliona uso wa nne ni wa ndama, huyu sura hiyo ameona ni ya kerubi. Sasa ukisoma kwa kurudiarudia hapa unagundua hapa kulikuwa na viumbe vya aina mbili, Makerubi na Maofanini (The wheels), ambao katika vitabu vingine vya kiyahudi wameelezewa na kutajwa sana.

🧚🏻‍♂ *MALAIKA/ANGELS*🧚🏻‍♂

🎴 Tunao msingi mmoja wenye makosa, nao ni kujiongeza wenyewe kuwa hao wote ni malaika, hiyo ni hatua ya kwanza kabisa ya uelewa kwamba viumbe vyote vya mbinguni ni malaika (malaika). Kwa mfano Maserafi ni Maserafi wala sio Maserafi ni Malaika, Biblia haisemi kamwe wala vitabu vingine vya kale, ni sisi tuliamua ku-generalize kuwa wote ni malaika tu, na baadhi ya watumishi katika kujaribu kusaidia uelewa, wakaamua kusema ni aina mbalimbali za malaika. Ingawa ukisema Serafi ni malaika umemshusha cheo kwa mujibu wa ile order of creation, yeye ameumbwa kama Serafi, kama Kerubi na sio malaika, wala viumbe hao hawafanani na malaika kwa mengi sanaaaaaa. Sasa malaika wako wa aina nyingi....

✍🏼  *MALAIKA WAKUU (ARCHANGELS)*

Wayahudi walitoka Babel na majina mengi ya malaika, lakini pia katika maandiko ya kiyahudi ya kale, yanataja malaika wakuu saba, kumbuka katika Daniel 10:13, Gabriel anamwambia Daniel kwamba akaja Mikael mmoja wa wakuu wasimamao mbele, kunisaidia. Hao wakuu tangu mwanzo ni hawa Anael, Gabriel, Mikaeli,, Raphael, Zakariel, Samael na Orifiel.

✍🏼 *MAJESHI YA MALAIKA/ARMIES*
🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂
🗡⚔🗡⚔🗡⚔💣💣💣🔥🔥
🎴 (Mathayo 26:53, 2Falme 6:14ff). BWANA YHWH anaitwa Bwana wa majeshi, anayo majeshi kama nilivyoeleza katika masomo yale (USHINDANI WA ROHONI & VITA VYA ROHONI, jitahidi uyapate hayo nimeyaandika mimi Mwl Proo). Sio malaika wote wanahusika na vita (battles), ndio maana kuna watu walistushwa na ule ushuhuda wa mwinjilisti wa Uganda kuwa katika matuo ya wakuu wa giza, walikuwa wanaweza hata kumteka malaika (hususani guardian angels, mimi hilo sishangai maana najua yaliyoko huko). Malaika wa kundi hili wako chini ya Mikaeli (ambaye jina lake lina maana ya "Kama Mungu"), wote wanapokea orders/instructions toka Mikaeli, kiasi cha kufanya waitwe malaika zake (Ufunuo 12:7-11), kama ambavyo malaika waliomcha Shetani huitwa malaika zake. Ukisoma katika maandiko majeshi ya BWANA, au matuo ya Bwana (forces of the LORD), inazungumzia kundi hili la malaika. Hawa wote mpaka mwonekano wao wako muscularly strong 💪🏾🗡 (always wako na drawn sword kwa mikono yao), hawa hutumwa mara kwa mara kulingana na ukubwa vita inayomkabili mtu au kanisa n.k, na kuna vita zingine wanapigana tu huko rohoni, (there is unceasing wrestling of spiritual forces kule rohoni, ni wachache wanaelewa haya, ndio maana watu wa Mungu hawapaswi kuacha kuomba siku zote day & night).

✍🏼 *WALINZI WA MBINGU (WATCHERS)*
🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂

🎴 Hili ni kundi jingine la malaika, ni tofauti kidogo na majeshi yale yaliyo chini ya Mikael ambayo specifically wao ni kwa ajili ya ushindani wa kivita. Hawa nao ni spirits of heaven, kama unasoma documents za kale, utakuwa umewahi kutana na visa vya hawa. Kwa mfano wale malaika 200 walioshuka katika mlima Hermoni zama zile za Vizazi vya mwanzoni baada ya Adamu, wakaingia kwa wanawake wa kibinadamu ni kundi hili hapa la *Watchers of Heaven*, waliongozwa na kiongozi wao Semjaza/Samyaza.

✍🏼 *MALAIKA WAKUU WA MIJI (PRINCES)*
🎴 Ufalme wa Mungu umejidhatiti kwa namna ya ajabu sana. Miji yote ina malaika/Prince(s), wa kuuchunga, na kama kuna mambo yoyote ya makusudi ya Mungu yanapaswa kutekelezwa basi yeye yuko in charge kwa kazi hizo. Yaani watu wa Mungu walipaswa kuwa na kiwango cha kutembea na Mungu kiasi cha kuweza kuwaona na kuwajua hawa. Nimefurahia ushuhuda wa Prophet Sadhu Selvaraj, akiwa Airport moja huko Marekani anasubiria flight ✈, akahisi kuna uwepo wa kiumbe karibu yake, akageuka na tazama kuna malaika yuko Giant mwenye upanga uliofutwa, akajitambulisha _*"I'm the Prince of this city"*_, na akamwonesha maeneo ambayo yatapatwa na tetemeko, ambapo Bwana Yesu alikuwa amekwisha mwonya mbele juu ya mji huo na uharibifu utakao tokea. Tusome maandiko

*(Ezekieli 9 )*
------------
_*1 Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake.*_
*_2 Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba._*

👆🏽👆🏽👆🏽👆🏽 These are angelic beings aliowaona Ezekiel, wametajwa kazi yao kuu ni kuusimamia mji. Kama kuna kusudi lolote la Mungu la kutekelezwa katika mji liwe baya au zuri, hawa watahusika kwanza.

✍🏼 *MALAIKA WALINZI/WALEZI WA WATU (GUARDIAN ANGELS*

🎴 Hili ni kundi jingine la malaika, hawa sasa wako so much involved na mambo ya wanadamu, ni Guardians, kama bodyguards hivi, wako kwa kila mwamini at least one. Wako kama reporters/wapelekao habari zetu kwa Bwana, uhusika na kuchukua majibu ya maombi katika kiti cha enzi na kumfikishia mhusika.

*_"Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni."_*
(Mathayo 18:10)

Unaweza kuona, wametajwa hapa malaika wao (guardian angels), wamakuwa na mtu, na kuna muda wao maalum hupeleka reports kwa Baba. katika Mhubiri 5:6, anaposema usimwambie huyo malaika kuwa umepitiliwa tu kufanya kosa fulani, anazungumzia guardian angels,na watu wa Mungu wanapaswa katika kiwango hata cha kuwaona hawa hata kamasio wakati wote.

*II MALAIKA WAASI NA MAPEPO/MAJINI*
🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂ versus 👹👹👹👹

🎴 Naomba kuweka sawa hoja kadhaa ambazo haziko sahihi, zinapishana na maandiko yaliyotangulia. Malaika waasi sio majini/mapepo wabaya hawa tunaowakemea watoke kwenye miili ya watu. Malaika waasi toka Mwanzo mpaka Ufunuo jina lao ni hilo Malaika waasi au Malaika za Shetani, na sio pepo wabaya/waovu. Malaika walioasi na Shetani wako katika maumbile yao ya asili 🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂, wamekosa utukufu wa Mungu tu maana wamejitenga na chanzo cha utukufu wao. Hawana masura hayo ya kutisha na mapembe 👹👹👹, wao kuna namna nyingi hawana tofauti na malaika walio watakatifu kwa Mungu, ukiacha na swala la utukufu wa Mungu ambao hawana. Tusome maandiko

*_"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."_*
(Waefeso 6:12)

👆🏽👆🏽👆🏽👆🏽 Hizi ranks za utawala wa Shetani, Mwovu, zimeainisha kitu cha muhimu sana.

1. Falme na Mamlaka
2. Wakuu wa giza/anga
3. Majeshi ya pepo wabaya

✍🏼 Sasa hizo ranks mbili za kwanza ni malaika waasi walioamua kushawishika na uasi wa Shetani juu ya Mungu, na yeye Shetani kawaweka kwa vyeo vya juu, anga ya mkoa mzima inaweza kuwa na mkuu wa giza mmoja na akachachafya kwelikweli, chini yake kutakuwa na majeshi ya pepo wabaya. Narudia tena malaika waasi sio hawa mapepo wabaya/waovu.

*PEPO  WABAYA WALITOKA WAPI??*

👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹
Hili ni swali la muhimu sasa kwetu. Jibu moja linakubaliwa na vyanzo vya kale vyote ni hili, *mapepo wabaya ni roho za wanefili waliokufa (spirits of dead nephilims)*, hili linathibitishwa na the Jubilee, The Book of Jasher, The Book of Enoch etc. Ukikutana na myahudi mkristo, ukamwambia pepo wabaya ni malaika walioasi ataona unafanya comedy.  Tusome kidogo andiko hili;

_*8. Now the giants, who lave been born of spirit and of flesh, shall be called upon earth evil spirits, and on earth shall be their habitation. Evil spirits shall proceed from their flesh, because they were created from above; from the holy Watchers was their beginning and primary foundation. Evil spirits shall they be upon earth, and the spirits of the wicked shall they be called. The habitation of the spirits of heaven shall be in heaven; but upon earth shall be the habitation of terrestrial spirits, who are born on earth 9. The spirits of the giants shall be like clouds, which shall oppress, corrupt, fall, contend, and bruise upon earth.  (Enoch 15:8-9)*_

👉🏾 🧚🏻‍♂ Malaika walioasi hawaitamani miili ya wanadamu, wao hawana shida ya habitations.

👉🏾 👹 Pepo wabaya ndio wenye uhitaji na makao/habitation, maana wao walipoteza ya kwao. Baba zao wanefili ambao ni malaika walioacha makao yao *Proper domain* waliyoumbiwa walikamatwa na kufungwa katika *Tartarus*(Underground gloomy dungeon) Soma 👉🏾 2Perto 4:4, Yuda 1:6, Enoch chapters 7-9. Hawa malaika waliofungiwa hapa sio wale walioasi na Shetani, wale hakuna aliyefungwa, na muda wao bado kabisa. Sasa roho za wale wanefili ambazo ni products ya spirits of heaven kuungana na terrestrial spirits ndizo zikaitwa pepo waovu. Hazina kikao (habitation), wao ndio hawa tunaokemea watoke kwenye miili ya watu. Malaika waasi wao kama managing directors watahakikisha wanawakosesha wanadamu ili kuruhusu hawa mapepo sasa yawaingie, ila sio wao. Ndio maana vyanzo vya kle vinakubaliana katika hili kuwa hakukuwahi kuna pepo wabaya (demons) kabla ya gharika ya Nuhu. Pepo hawa ambao hawakuwa katika ratiba za uumbaji wa Mungu bali ni matokeo ya makosa ya malaika, wanasifa kadha wa kadha, mfano wanao uwezi wa kuji-multiply kiidadi.

👉🏾 Hizi roho za kipepo (demonic spirits), hazina sifa za roho za mbinguni kwa 100% ila their foundation is of heaven. Hazina ulinganifu na roho za wanadamu, na ndio maana hazina makao. Roho za wanadamu waliokufa kwa gharika kuna mahali zimehifadhiwa, ila hizi hazikustahili kwenda hata kule.

👉🏾 Wanefili wali-express tabia zote za hawa pepo wachafu wakiwa katika miili yao. Walileta kila ubaya, wali-exhaust chakula cha wanadamu, wakaanza kula mpaka wanadamu. Walitenda dhambi juu ya wanadamu, haikutosha wakaanza kuwaingilia hata wanyama, waliidhuru hata mimea, hakuna kilichobakia salama. Sasa gharika iliua wanadamu wote kasoro nane tu, na wanefili waliuawa, ila roho zao sasa zikawa pepo wabaya (Eno 15:8-9). Na kinachotokea ni nini, hizi roho zao zinatamani ku-express zile tabia zao, lakini they cannot kwa kuwa hawana miili chombo cha kuruhusu utendaji duniani. Hivyo mapepo yatafanya kila linalowezekana yapate makao ndani ya mwili wa kiumbe hai hususani mwanadamu, ili yapate fursa ya kufanya yao. Tabia zinazofanywa na wanaomilikiwa na pepo ni zilezile zilizokuwa zikifanywa na wale majitu na kuzidi sana.

👉🏾 👹👹 wanaweza kujivika sura tofautitofauti, lakini haya masura ya ajabuajabu ndiyo ya kwao, maana roho hizi sio wale malaika waliowahi kumtumikia Mungu mbinguni. Kuna jambo moja lisilojulikana sana kwa wasomaji wa Biblia pekee, nyakati za yale majitu kulitokea viumbe ambao ni *hybrid*, waliokuwa ni mchanganyiko wa species za wao majitu na wanyama, na watu etc etc, ikatoa viumbe hata majina hawana, wana maumbile ya ajabu ajabu. Na sehemu kubwa ya mapepo hupenda kuchukua sura zile za viumbe visivyoeleweka. Mimi nilipata kuona pepo kwa macho ya roho kwa ghafla nikiwa bwenini miaka 14 iliyopita, lilitokea dude kubwa lenye mikia kama pweza pande zote, likapotea kupitia ceiling board. Pepo wachafu (ambao kiarabu ni Jinn/Majini) wanazosifa zingine nyingi ambazo sitapenda kuweka hapa kwa sasa, maana hatupaswi kuyajua haya kuliko tunavyojua mambo ya upande wa nuru.

*III ROHO ZA WANADAMU*

🎴 Naweza kusema hapa ni mwanzo wa moyo wa somo. Leo tupate ujuzi huu, ili tuweze kuishi kwa standard sahihi tungali hai hapa duniani. Roho ya mwanadamu iliumbwa kwa namna ya roho zingine, lakini haikupewa uwezo sawa na roho za mbinguni. Pia roho ya mwanadamu inapokuwa ndani ya mwili wa udongo inakuwa kama imefunikizwa fulani, na kushindwa ku-opereti kama roho kwa 100%, ikiweza kuushiriki ulimwengu wa roho basi ni kwa njia ya maono, ndoto au roho kuondoka (sio kwa kifo), na hapa kuna namna nyingi kama nilivyoelezea katika somo langu la *MWILI WA ROHO*, nimeliandika mimi Mwl Proo, waweza kulipata. Hivyo roho za wanadamu zinahitajika kuwezeshwa, ili kutenda kazi katika limwengu za kiroho na kuoperet kwa viwango vya juu hata kama iko ndani ya mwili wa udongo. Wengi wenu mnaweza kuogopa mambo ya roho kusafiri (levitate/astral travel), nami siji kukihimiza hicho, ila naelekeza kitu cha kibiblia kwa manufaa ya watu wa rohoni (1Korintho 2:14-15). Kuna viwango ukitaka kutenda kazi za kiroho lazima roho iwezeshwe (iwe enhanced/enabled). Mwanadamu anao mwili (unakua 👉🏾 GROWTH), anayo nafsi (inahitaji kujengwa 👉🏾 edification 1Kor 14:4), na anayo roho (hii inahitaji kuongezeka nguvu na kuwezeshwa 👉🏾 Luka 1:80, 2:40). Roho inaongezeka nguvu na kuwezeshwa, inaweza kuwa kwa Roho wa Mungu au kw uwezo wa kishetani (Mika 3:8). Mwanadamu anao uwezo wa kufanya mambo makubwa sana akiwa katika mwili,akaoparet kiroho, akaona vitu vya rohoni, akawasiliana na viumbe vya rohoni, anaweza kuhisi kila linaloendelea rohoni kwa roho yake iwapo imewezeshwa. *The Spirit enables spirits*, siku ambayo Mungu alinifundisha hili kwa Roho Mtakatifu, niliomba Mungu anipe experience ya hiki kitu kilivyo halisi. Tangu hapo nimekuwa na maombi ya kuomba jambo hili, tayari linafanya kazi kwa sehemu lakini bado kabisa shauku yangu ni kubwa. Siku nilipoomba Mungu aiwezeshe roho yangu ili niongezeke viwango vya kutenda kazi na kuenjoy maisha ya kiroho, niliweza kusikia majadiliano ya watu ambao wapo mbali sana. Nikiwa Dar es Salaam nilisikia mazungumzo ya watu ambao wapo Kagera, ni kama nipo katikati yao. Kuna siku moja baada ya kumaliza maombi ya usiku nikalala tena, na baada ya muda nikamwona adui ananishambulia na kujificha, kisha nikaona ni kama nipo pembeni ya mwili wangu na adui anaubana ule mwili, ila na mimi kwa roho yangu nahisi kule kubanwa, sema nilikwisha jua somo hili ninalo andika, hivyo nikiwa katika hali hiyo roho yangu iliomba, nikimsihi Mungu nitie nguvu roho yangu ili nimshughulikie yule adui, Mungu alijibu kwa kutenda, kwa sekunde chache yule  adui nilimsambaratisha kabisa. Ziko karama za Roho Mtakatifu zinaweza fanya kazi ndani ya mtu iwapo roho yake imewezeshwa. Unaweza kuangalia baadhi ya watumishi wa Mungu, ukaona kutenda kazi kwao kukakutatiza, kumbe roho zao ziko *enhanced* kutenda hayo. Roho ya mwanadamu ikiwezeshwa inampa mwanadamu huyu kuweza kutumia miliango ya fahamu ya kiroho zaidi, roho ina masikio, ina macho, ina ngozi etc. Mtu ambaye roho imewezeshwa anaweza kuingia mahali pepo mapepo akaya-sense kwa moyo tu, na kuna hatua mpaka kwa mwili. Muda wote tumezungukwa na tupo *exposed* kwa viumbe wa kiroho, wawe wema wa Mungu au wabaya wa Shetani, wapo tu wamejaa, shida ni macho ya kuwaona yamefumbwa, kwa sababu roho ikiwa ndani ya mwili wa udongo inakuwa limited/restricted. Lakini ikiwezeshwa unaweza ona vyote vya rohoni, malaika wakishuka unawaona, kwa hatua ya awali at least you sense their presence.

👉🏾 Namfahamu muhubiri ambaye muda wa kuhudumia wenye mahitaji, wale wagonjwa na wenye shida wote anawaona mara mbili, anamwona mtu wa mwilini na wa rohoni kwa pembeni. Kwa hiyo akiombea kiwete ♿, akisema *you're free*, anakuwa amemwona yule wa rohoni keshasimama. Namfahamu mhubiri ambaye akiwa anafundisha hata kama yuko ofisini kwake anawaona malaika waliopo muda huo hapo ofisini, idadi yao, mavazi yao na kila kitu. Macho ya roho yake yametiwa nuru (Efeso 1:18), wengi wanatenda kazi na malaika lakini hawajui kwa kuwaona wala kwa ku-sense. Roho ikiwezeshwa maisha ya kiroho yanakuwa matamu zaidi, kwa sababu hakuna jambo litatokea ukiwa hujalipata kabla hata kama ni mambo ya kawaida yasiyo ya kiroho ila yanagusa maisha yako na kuweza kuleta athari au matokeo fulani, lazima utayapata kabla, roho inayouwezo wa ku-sense uwepo wa ajali, kifo, ugonjwa unaokuja, kupoteza kitu, baraka inayokuja, hata kama mchana wa kesho kuna kosa utafanya roho inaweza kuli-sense kosa hilo siku moja kabla, labda uwe mpuuziaji tu. Ndio maana nahimiza juu ya roho kuwezeshwa kwa Roho wa Bwana.

3⃣ *TAFSIRI YA LUGHA ZA ROHO*

🎴 Mapenzi makamilifu ya Mungu ni kusema nasi waziwazi bila mafumbo (without riddles). Sasa lugha ya kinabii imejaa mafumbo ya alama (Symbols & Signs). Watu wakiona maono au ndoto au maono ya wazi, wanaona vitu kwa lugha ya mafumbo yenye alama au viwakilishi.

*NB:*
_*Vitu vya kiroho ni vya kiroho mwilini, lakini ni vya kimwili rohoni. Yaani pepo mchafu ni wa kiroho huku mwilini, haumwoni, lakini ukiingia rohoni lile pepo ni la kimwili unaweza kumwona na anaonekanaje kwa umbile.*_

🎴 Vitu vya rohoni vinawekewa alama *(Encoding)*, kwa sababu roho ikiwa katika mwili haiwezi kufanya kazi katika roho 100%, na hivyo huwezi yaona mambo kama yalivyo, bali taarifa zinakuwa *encoded*, na kazi kubwa inayotakiwa hapo ni ufahamu wa rohoni kwa Roho Mtakatifu uweze ku *decode*, yaani zile taarifa zilizokuja kwa uwakilisho wa alama za mafumbo kuzitafsiri tena kuwa taarifa. Nakumbuka nilikuwa kwenye Conference ya wanafunzi, mhubiri muda anataka kuhudumia vijana kwa maombi aliita mabinti, akiwa anamwuliza Roho wa Kristo awaombee nini, ghafla akaona katika roho 👉🏾🌙🌘 mwezi, akasema Roho ananionesha mwezi sijui ni nini, muda huohuo akapata tafsiri kuwa wadada waliofika pale wengi wanashida katika Menstrual Periods zao na kifungo cha kipepo kimekaa hapo. Alipoomba pepo wachafu wakapiga kelele wakikiri waliwashika matumbo ya uzazi kupitia siku zao za hedhi. Ona jinsi ambavyo isingewezekana aone sehemu ya wadada na shida yao ikoje, lakini taarifa imekuja ikiwa imefungwa kwa alama ya mwezi 👉🏾🌘🌙 (encoded) na roho iliyowezeshwa inaweza ku-decode ili kutafsiri hilo fumbo la alama. Ndivyo ilivyo kwa lugha zote za rohoni. Lakini roho ya mwanadamu ikiwa rohoni kwa zaidi ya 90% haioni mafumbo, inaona mambo katika uhalisia wake. Nakusihi endelea kufuatilia masomo yangu ya siku za usoni, nitaweka kwa kina mambo ya hizi lugha za rohoni na swala zima la *ENCODING AND DECODING*, Ili usiwe mtumishi mpumbavu kwa kuona mengi ukashindwa kuyaelewa na kuyatia moyoni (Isaya 42:20).

4⃣ *NAMNA YA KUIFANYA ROHO YAKO IWEZESHWE*

🎴 Knowledge is power (ujuzi ni nguvu), kuyapata maarifa haya ni hatua ya kwanza na ya msingi sana. Wapo ambao kwa neema ya Mungu walijikuta tayari wanatenda kazi kwa viwango fulani vya kiroho na roho zao ziliwezeshwa kwa viwango fulani.

👉🏾 Wako ambao malezi ya kiroho waliyoyapata, na yale waliyoyasikia mara kwa mara, yalikuwa na mafundisho ya viwango ambavyo viliruhusu roho zao ziwezeshwe. Maana walitembea katika kina cha maarifa ya kiroho,na ikatoa mwanya huo.

👉🏾 Wako ambao waliambukizwa tu (spiritual impartation) sawa na Hesabu 11:16-17, na wakaanza kutembea na roho zilizowezeshwa.

👉🏾Mko wengi katika mnaosoma ambao sharti baada ya kupata maarifa haya, mwingie katika hatua ya kuyataka haya kwa BWANA (1Korintho 12:31). Ukianza kuomba kwa juhudi utafika katik kiwango kizuri cha kutenda katika roho, mimi pia sijafika natia juhudi katika kuzitaka karama zilizo kuu na haswa hili nililofunuliwa na Bwana.

👉🏾 Anza kutamani kuishi maisha ya mtu wa rohoni, tamani kuona katika roho, kusikia katika roho, kuhisi kwa roho. Sehemu kubwa ya maombi yako yawe ni kuomba vipawa vya rohoni na sio mahitaji ya mwili zaidi.

👉🏾 Tumia muda mwingi binafsi mbele za Mungu (Isaya 51:2), majra ya kuwa peke yako mbele za Mungu, tena muda wa kutosha ni mlango mzuri sana wa kuifanya roho yako iwezeshwe. Maana ni ngumu kumtumikia Mungu ambaye ni roho ukiwa haupo rohoni,au ukawa mgeni wa mambo haya nisemayo.

👉🏾 Jifunze kwa watumishi ambao wanaopearet katika limwengu za kiroho, ili kuku-equip kwa maarifa muhimu, wako waliofuata mambo ya kiroho bila maarifa wakapitea kabisa, wakaishia kuongozwa na pepo wachafu tu wakidhani ni Mungu.

*MUNGU AKUBARIKI KWA KUSHIRIKI NEEMA HII YA KUPATA MAFUNDISHO. KUNA MAMBO MENGI NIMEYAONDOA NA SOMO NIMELIKATISHA KWA KUWA NI REFU SANA, NITAENDELEA KUYAANDIKA KATIKA MASOMO YAJAYO

Thursday, 13 September 2018

MAISHA MAZURI NI YAPI? (What is the Good life?)



MAISHA MAZURI NI YAPI?
(What is the Good life?)
“Living well”
Je ina maana gan tunaposema kuishi vizuri,(maisha mazuri). Ina maanisha nini kusema maisha ni mazuri?
Kila mtu anapenda kuishi maisha mazuri hakuna anayependa kuishi maisha mabaya.Lakini swali hili si rahisi kama jinsi lilivyo.kuna namna nyingi jinsi wanavyo tafsiri kuhusiana na maisha mazuri.wengi wametafsiri maisha mazuri kama ifuatavyo
MAISHA YENYE MAADILI
Njia mojawapo tunayotumia kwa neno uzuri au nzuri.Ni kuthibitisha maadili mema au mazuri.Kwa hiyo tunaposema mtu anaishi vizuri au watu Fulani wanaishi vizuri tunakuwa tumemaanisha :-
Mtu mwenye kutia moyo,mstaarabu,mkweli,mwaminifu,mpole,anaesaidia wengine.wana fanya vitu vyote vyenye asili ya wema na ubinadamu.
Na hawatumii muda wao wote kufanya wanayoyapenda tu bali husaidia na wengine.Baadhi ya wanafalsafa wanasema ni bora kuishi maisha ya tabu wakati ukitenda mema kuliko kutenda mabaya.Kwamba mtu mwema ni yule anayepata tabu kiasi cha kufa kwa kutenda mema kuliko mtu tajiri ambae anatenda yasiyo faa.
Dini nyingi hutafsiri maisha mazuri ni yale yenye maadili mema na kuishi kulingana na amri za Mungu.Mtu anaeyeishi maisha haya hutii amri za Mungu na kufanya yanayostahili.Na huamini kuwa malipo ya wafanya mema yako mbinguni na yawafanya mabaya yapo hapa  hapa duniani au maisha baada ya kifo
MAISHA YA FURAHA
Kitu kinachofanya maisha kuwa na thamani ni kuishi maisha ya furaha.maisha ni kufurahi na kuburudika,mtazamo kuwa maisha ni furaha hufanya maisha kuwa na uthamani wake.
Mtu anaposema ana furaha ana maanisha anajisikia vizuri,na maisha mazuri yamefungamana na mfululuzizo wa kujisikia vizuri mda mwingi.maisha mazuri yanatakiwa kuwa ni yale yenye furaha.kuwa na marafiki wazuri na washauri wazuri husaidia mtu kuwa na furaha.
MAISHA YALIYO KAMILIKA
Kila mtu anahitaji kuwa na furaha ,tunathamini vingine kwa sababu vina maana kwa vitu vingine kwa mf:-
Tunathamini fedha kwa sababu hutusaidia kununua vitu tunavyo vihitaji.Baadhi ya watu huamini ukamilifu wa kila kitu katika maisha huleta kuwa na maisha mazuri,mf gari,nyumba, watoto n.k,kuna tatizo katika kufikiria katika mtizamo huu.Kuna watu wana ishi maisha ya burudani/starehe wakati wote, je tuwahesabu kuwa wanaishi “maisha mazuri”?.Wanafalsafa wengi wanakubaliana kwanza kwamba kuishi maisha mazuri kwanza ni lazima mtu awe na tabia njema ,au utu wema.Na pia hatuwezi kusema mtu anaishi maisha mazuri kama anapatwa na matatizo au shida mara kwa mara. Na sio tu vile mtu anavyojisikia yeye mwenyewe kuwa na furaha.Kuna baadhi ya mitazamo  ina bidi iwepo ili kuhesabu mtu ana maisha mazuri mf:-
AFYA: Binadamu lazima afurahie afya bora na kuishi muda mrefu.
MARAFIKI: Binadamu lazima awe na marafiki wazuri,kawaida ya binadamu ni kuhusiana na wengine kwa sababu hiyo kuwa na marafiki ni jambo la muhimu sana.
Ni lazima mtu kupata heshima kutoka kwa wengine bila kuangalia hali wala jinsia ,kuwa maarufu na mtu mwenye sifa sio kitu cha lazima.Uthamani wa mtu haupimwi kwa umaarufu alio nao,bali hupimwa na kutambulika na watu wanao mzunguka.
Ni muhimu kufanya yale yaliyomo kwenye uwezo wako,na kitu kitu kinacho mtofauticha binadamu na wanyama wengine ni juu ya kufikiria na kufanya maamuzi,kwa hiyo maisha mazuri pale mtu pia anapofanya yale yaliyopo ndani ya uwezo wake katika kuyafanya na kuyatenda.
MAISHA YENYE MAANA
Tafiti nyingi zimeonesha kuwa watu wenye watoto sio wote wenye furaha,ukilinganisha na wale ambao hawana watoto.Wakati wa ukuaji wa malezi kwa mtoto hasa pale watoto wanapofikia umri wa kupevuka wazazi huwa na kiwango kidogo cha furaha na huongeza kiwango cha mawazo.Japo kuwa na watoto ni kigezo cha kuwa nafurha lakini haifanyi kuwa chanzo cha maisha yenye maana.Wakati wa zamani kuwa na watoto wengi ilikuwa ni kitu cha kujivunia tena chenye ufahari lakini pale tu inapotokea kila mtoto kufanikiwa katika njia yake pale fahari hujitokeza lakini pia sio maana halisi ya kuwa na maisha mazuri.
Wagiriki wana msemo kuwa “usimuite mtu ana furaha mpaka awe amekufa” Huwezi kusema mtu ana furaha mpaka mtu huyo maisha yake yawe yamefika kikomo,haijalishi mtu ana furaha kiasi gani kwa sasa kitu kibaya chaweza kumtokea na kuharibu furaha yake.Mtu kumuhesabu kuwa na furaha ni mpka pale tutakapoona mwisho wa maisha yake umeishaje.”heri mwanzo mbaya kuliko mwisho mbaya”
Jimmy savile,Ni mtangazaji  wa BBC aliyekuwa na umaarufu mkubwa na watu walimpenda sana kutokana na kazi yake na aliipenda kazi yake alifanikiwa sana kutokana na kazi yake,alikuwa na marafiki wengi na watu walimheshimu.Lakini baada ya kufa ili fahamika kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa akiongoza genge la uzalilishaji wa kijinsia hasa kwa watoto.Kwa hiyo mbele ya watu alionekana kuwa ni mtu mwenye maisha mazuri lakini mwisho wa kifo chake ikafahamika alikuwa na makosa ya udhalilishaji wa kijinsia(serial sexual predator).Yamkini alifurahia maisha yake,Lakini ukweli hakutaka kusema kuwa alikuwa anaishi maisha mazuri au la.UKWELI MAISHA MAZURI NI YALE YAKUPENDEKA  NA YANAYOHITAJIKA KATIKA KILA NYANJA  AU YOTE YALIYOELEZWA HAPO

Sunday, 27 August 2017

Nafasi za kazi mwisho wa kuapply ni 30/08/2017

 BONYEZA LINK IFUATAYO KWA MAELEZO ZAIDI
ajira

NAFASI MBALI MBALI ZA KAZI KUTOKA SERIKALINI

Bonyeza link zifuatazo kwa maelezo zaidd

Ajira muhimbili

NAFASI YA KAZI SERIKALINI MDAs

TANGAZO KWA WAOMBAJI KAZI WALIOITWA KWENYE USAILI WA TRA.

Waombaji kazi waliotwa kwenye usaili wa kada mbalimbali za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanasisitizwa kuwa hakuna utaratibu wa kuomba kubadilishiwa kituo cha kufanyia usaili ambacho mwombaji kazi amepangiwa.
Usaili huo ambao utafanyika katika Vituo kumi hapa nchini, vimepangwa kwa kuzingatia anuani za waombaji ambazo waliainisha kwenye barua zao za maombi ya kazi, hivyo mgawanyo wa vituo vya kufanyia usaili huo umezingatia ukaribu wa Mikoa kwa kila kanda ili kuwaepushia usumbufu wasailiwa kusafiri umbali mrefu.
 Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano,

Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma 25 Agosti, 2017.

UMUHIMU WA KWENDA CHURCH


Kwa mtu MKITRO ni lazima kuhudhuria kanisani. Sio tu kwa sababu ni kitu kinachompendeza Mungu, bali pia ni kwa ajili ya kukua na kuimarika kiroho. Kuna sababu nyingi za kiMungu zinazotufanya tuhudhurie ibada kanisani, hapa kuna baadhi ya hizo

1. Ni udhihirisho wa upendo wetu kwa Mungu

Kuhudhuria ibada kanisani ni udhihirisho halisi na unaoonekana wa
 upendo wetu kwa Mungu. Ni mahali tunapoweza kumtolea Mungu dhabihu za sifa, shukrani na heshima.

Zaburi 134:2 Inueni mikono yenu katika mahali patakatifu
na mumsifu BWANA .

Tunapaswa kumtolea Mungu muda na nguvu zetu katika kumwabudu na kumsifu maana yeye pekee ndiye anayestahili.

Ufunuo 4:11 Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ni wewe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako vitu vyote viliumbwa na vinapata kuwapo.”

2. Tunaimarika Kiroho

Tunaposikia neno la Mungu likihubiriwa na kufundishwa kanisani imani yetu inakua na roho zetu zinaimarika. Ni muhimu kwa roho zetu kuwa na akiba ya neno la Mungu la kutuwezesha kuvuka pale tunapokutana na changamoto mbali mbali. Ni muhimu kutumia kila nafasi tunayoipata kujivika silaha za Mungu ili tuweze kumshinda adui, na tunapohudhuria kanisani tunapata kulishwa neno la Mungu, kutiwa moyo na kuimarishwa roho zetu. Neno la Mungu ndilo linatuimarisha na kujenga imani yetu.

Warumi 10:17 Basi, chanzo cha imani ni kusikia, na kusikia huja kwa kuhubiri neno la Kristo.

3. Tunapata nafasi ya kuwa katika uwepo wa Mungu


Kuna ahadi ya Mungu kuwa wakutanapo wawili au watatu yeye anakuwa kati kati yao, watu wanaojihudhurisha pamoja kwa ajili ya kumtafuta. Pamoja na kwa Yesu yupo ndani yetu, anadhamini sana mkutaniko wa watu wanaokutanika kwa ajili ya kumuomba, kumsifu, kumuabudu na kumsikiliza. Mahali kama hapo Mungu anashusha uwepo wake, upako na nguvu zake.

Mathayo 18:20 Kwa maana wanapokutana watu wawili au watatu katika jina langu, hapo mimi nipo pamoja nao

Na katika uwepo hu wa Mungu, Roho Mtakatifu anashusha vipawa vyake na karama mbalimbali.

4. Inaleta umoja katika kanisa la Mungu
Tnapokutanika pamoja kwenye ibada tunapata kufahamiana na wapendwa wengine na kuleta umoja miongoni mwa watu tunaomwamini Mungu. Uhusiano mzuri na Mungu unahitaji pia kuwa na uhusiano mzuri na watu wa Mungu. Huwezi kumpenda Mungu na kumchukia ndugu yako.

1 Yohana 2:9-10 Mtu anayesema kwamba anaishi nuruni, naye anamchukia ndugu yake, bado yumo gizani. 10Anayempenda ndugu yake anaishi katika nuru na wala hana kitu cha kumfanya ajikwae

Huwezi kuwa na uhusianao na watu usiowajua wala kukutana nao hivyo kwenda kanisani kunakupa nafasi ya kukutana na kufahamiana na watu wa Mungu.

1 Yohana 1:7 Bali tukiishi nuruni, kama yeye alivyo nuru, tunakuwa na ushirika sisi kwa sisi na damu ya Mwanae Yesu, inatutakasa dhambi zote

5. Ni ishara ya utii kwa Mungu
Kwenda kanisani ni ishara ya kuonyesha utii kwa Mungu na kwa neno lake. Neno la Mungu linatuasa tusiache kukutanika pamoja.

Ebrania 10: 24-25 Na tujishughulishe kutafuta jinsi ya kuhimizana katika kuonyeshana upendo na kutenda mema. Tusiache kukutana pamoja, kama wengine wanavyofanya, bali tutiane moyo, hasa zaidi tunapoona siku ile ikikaribia.

Kukutanika huku kunatupa nafasi ya kuimarishana, kutiana mouo, kuinuana na kufarijiana na wapendwa wengine. Ukifahamu umuhimi wa kenda kanisani nawe ukawa hufanyi hivyo utakuwa unamkosea Mungu.

Yakobo 4:17 Mtu ye yote anayefahamu lililo jema kutenda, lakini asilitende, basi mtu huy
anatenda dhambi.

MUNGU akubariki ana.
Neema za Kristo.

Saturday, 26 August 2017

MKUTANO MKUBWA WA INJILI TANGA

CASFETA TAYOMI mkoa wa TANGA imekusudia kuwa na mkutano mkubwa wa injili,utakao fanyika katika wilaya ya korogwe mkoani humu,hii itahusicha matawi yote ya mkoa wa TANGA yale ya sekondari na ya vyuo vikuu.Wana CASFETA TAYOMI wote Mkoa wa Tanga wana karibishwa kuhudhuria Mkutano huo
Mkutano huo utakuwa ni wa siku saba (7),pamoja na mahubiri kutakuwa na kwaya Mbali mbali zitakazo hudumu katika mkutano huo.na Wakati wa usiku kutakuwa na sinema itakayo kuwa inaoneshwa.
Wagonjwa na wenye shida mbalimbali wataombewa na watawekwa huru katika jina la Yesu.