Thursday, 6 October 2016
HISTORIA YA UKRISTO DUNIANI (2)
Ujio wa Roho
Mtakatifu
Mara baada ya
Yesu kwenda zake katika tukio linalotajwa kupaa kwake mbinguni, wafuasi wake
wakarudi Yerusalemu, yapata mwendo wa sabato, na walipoingia huko, wakapanda
ghorofani walipokuwa wakikaa Mtume Petro na wenzake.
Hata ilipotimia
siku ya Pentekoste walikuwapo wote mahali pamoja. Ukaja upepo toka juu kama
upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
Kukatokea na ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja
wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama
Roho alivyowajalia. (Mdo 1:12-14, 2:1-4).
Hii ilifuatiwa
na Petro na wenzake kuanza kuhubiri ufufuko wa Bwana Yesu na hatimaye kugusa
watu 3,000 waliokubali kubatizwa siku hiyo. (Mdo 2: 37-40).
Ustawi wa jumuia
ya kwanza ya wafuasi wa Kristo
Watu walipokuwa
wakidumu katika fundisho la mitume, sala, kumega mkate na katika ushirika,
wengi wakaona ishara zao nyingi basi nao wakauza mali zao, na vitu
walivyokuwanavyo, na kugawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.
Basi, siku zote
kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakila pamoja na kushiriki kwa moyo
mweupe.
Hivyo ndivyo
jumuia ilivyozaliwa na kufahamika kama Kanisa. (Mdo 2:42-47).
Kukutanika na
kushiriki mafumbo makuu, kushukuru na kusifu, pamoja na uwepo wa vipaji na
karama za Roho Mtakatifu, hufanya Kanisa liwe hai.
Uenezi wa Kanisa
Ujumbe wa Yesu
ulienea haraka toka Yerusalemu hata Lida, Yafa, Kaisaria, Samaria, Damasko n.k.
na kuanzisha jumuia nyingi.
Basi ukaja
wakati ambao Wakristo wakaanza kukosoana kuhusu dhamiri zao na huduma. Ndiyo
asili ya nyaraka mbalimbali ambazo zinaunda sehemu muhimu wa Agano Jipya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment